Dodoma FM

UMISETA wahimizwa nidhamu

7 June 2023, 4:19 pm

Wanafunzi 115 wa shule za sekondari wilayani Kongwa wanaoshiriki mashindano ya umoja wa michezo kwa sekondari UMISETA wakiwa katika viunga vya ofisi ya mkuu wa wilaya Kongwa. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Afisa usalama wilaya ya Kongwa Bwana Mwakasendo amesisitiza kuzingatia muda na kuwa wavumilivu kuendana na ulimwengu tulionao kwani muda ni siri ya ushindi.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Wanafunzi 115 wa shule za sekondari wilayani Kongwa wanaoshiriki mashindano ya umoja wa michezo kwa sekondari UMISETA wametakiwa kudumisha heshima, nidhamu na kuzingatia mambo ya msingi waliyoelekezwa na walimu wao wa michezo.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kongwa Dkt. Omary Nkullo alipokuwa akiwaaga wanafunzi hao kuelekea kwenye mashindano ya UMISETA mkoani Dodoma ambapo amesema kuwa anatarajia ushindi kutoka kwao.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kongwa.
Mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kongwa wakiwaaga wanafunzi wa UMISETA. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel ameunga mkono suala la nidhamu na kuongeza kuwa anathamini umuhimu wa michezo kwani ni chanzo cha ajira na afya njema.

Sauti ya Mkuu wa wialaya ya Kongwa.

Aidha Mwema amewataka wanafunzi hao kumtegemea Mungu katika mazoezi na mashindano hayo ili waweze kufanikiwa zaidi.

Sauti ya Mkuu wa wialaya ya Kongwa.