Dodoma FM

Serikali yatenga zaidi ya milioni 725 kuzuia, kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza

7 June 2023, 6:18 pm

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akijibu swali hilo Bungeni Jijini Dodoma . Picha na Bunge Tanzania.

Dkt. Mollel amesema hayo, leo Juni 7, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Bernabetha Kasabago Mushashu katika Bunge la kumi na mbili Mkutano wa kumi na moja kikao cha 42, Jijini Dodoma.

Na Alfred Bulahya.

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2022-2023, Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga zaidi ya Milioni 725 kwaajili ya kutekeleza Mpango Mkakati wa tatu wa kitaifa wa kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza nchini.

Amesema, “katika mwaka wa fedha 2022-2023, Serikali Serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 725 kwaajili ya kutekeleza Mpango Mkakati wa tatu wa kitaifa wa kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza 2021-2026 nchini, huku mikakati mahususi ya udhibiti visababishi vya magonjwa hayo yasiyoambukiza.”

Sauti ya Naibu Waziri wa Afya .

Pia, Dkt. Mollel amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuongeza kasi kwenye eneo la upatikanaji wa dawa katika zahanati na vituo vya afya, idadi ya dawa, vifaa na vifaa tiba ngazi ya Zahanati imeongezeka kutoka aina 254 mwaka 2015 hadi kufikia aina 451 mwaka 2023, huku ngazi ya Kituo cha Afya ikiongezeka kutoka aina 414 mwaka 2015 hadi kufikia aina 828 mwaka 2023.