Dodoma FM

Wananchi wahimizwa kufanya utalii wa ndani

6 June 2023, 4:23 pm

Afisa uhifadhi kutoka hifadhi ya Mpanga Kipengere iliyopo katika mikoa ya Njombe na Mbeya Bw. Jamali Kilavo. Picha na Alfred Bulahya.

Dhana ya wananchi ya kuamini utalii hufanywa na watu kutoka nje ya nchi inakwamisha sana sekta ya utalii nchini.

Na Alfred Bulahya.

Kuelekea siku ya maporomoko ya maji duniani, watanzania wametakiwa kuacha kuamini kuwa suala la utalii linafanywa na watu kutoka mataifa ya nje pekee na badala yake wajenge utamaduni wa kufanya utalii wa ndani katika hifadhi mbalimbali za taifa.

Wito huo umetolewa leo na afisa uhifadhi kutoka hifadhi ya Mpanga Kipengere iliyopo katika mikoa ya Njombe na Mbeya Bw. Jamali Kilavo, wakati akizungumza katika kipindi cha The Morning Power show kinachorushwa na Dodoma Tv.

Amesema dhana hiyo imekuwa ikikwamisha ukuaji wa sekta ya utalii nchini huku mkuu wa uhifadhi kutoka hifadhi hiyo Donasian Makoi akieleza maandalizi ya maadhimisho ya siku ya maporomko ya maji duniani inayotarajia kuadhimishwa Juni 16 mwaka huu.

Sauti ya Afisa Uhifadhi kutoka hifadhi ya Mpanga kipengere .