Dodoma FM

Dkt. Mpango ahimiza wananchi kuendelea  kupiga vita matumizi mifuko ya plastiki

5 June 2023, 7:11 pm

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza katika kilele cha siku ya Mazingira leo. Picha na Fred Cheti.

Juni 5 ya kila mwaka ni siku ya mazingira duniani, sikuu hii inaadhimishwa kuhusu umuhimu wa mazingira kwa maisha ya binadamu.

Na Fred Cheti

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka Watanzania kuendelea kupiga vita matumizi ya mifuko ya plastiki na kuimarisha utunzaji wa mazingira ya vyanzo vya maji katika maeneo yao.

Kauli hio imetolewa leo jijini Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani yenye kaulimbiu ya “Shinda uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za Plastiki” yaliofanyika katika eneo la soko la wazi la Machinga.

Sauti ya Makamu wa Rais.
Viongozi wakishiriki katika zoezi la usafi mapema hii leo katika soko la Machinga complex jijini Dodoma. Picha na Fred Cheti.

Aidha Makamu wa Rais, ameziagiza halmashauri zote nchini kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo za utunzaji wa mazingira na kuandaa utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameleezea shughuli mbalimbali zilizofanyika katika kuelekea kilele hicho cha maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani jijini Dodoma

Sauti ya Mhe. Dkt. Selemani Jafo.

Akitoa salamu za mkoa wa Dodoma  mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wakuu wa wilaya wamekuwa wakitekeleza maagizo mbalimbali ya kusimamia utunzaji wa mazingira na kulinda vyanzo vya maji.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma .