Dodoma FM

DC Gondwe aagiza miradi ya BOOST kukamilika kwa wakati

5 June 2023, 5:56 pm

Mhe gondwe alipokuwa akikagua ujenzi wa shule mpya Bahi misheni. Picha na Bernadi Magawa.

Pia alitembelea jengo jipya la benki ya NMB wilaya ya Bahi ambalo tayari limekamilika na linatarajiwa kuanza kutoa huduma muda wowote.

Na Bernad Magawa.

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mheshimiwa Godwin Gondwe ameagiza miradi yote ya miundombinu ya elimu wilayani humo inayotekelezwa kwa fedha kutoka serikali kuu (BOOST) kukamilika kwa wakati kadri ya maelekezo ya serikali.

Gongwe ameyasema hayo mwishoni mwa mwezi uliopita alipofanya ziara ya kutembelea baadhi ya miradi hiyo akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bahi pamoja na wakuu wa idara, taasisi za serikali na uwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi.

Sauti ya Godwin Gondwe – Mkuu wa wilaya ya Bahi.

Pamoja na kutembelea miradi hiyo, mheshimiwa Gondwe pia alitembelea jengo jipya la benki ya NMB wilaya ya Bahi ambalo tayari limekamilika na linatarajiwa kuanza kutoa huduma muda wowote na kujionea uwekezaji mkubwa wa huduma za kifedha ndani ya wilaya hiyo.

Akikagua ujenzi was shule mpya ya msingi Bahi Misheni. Picha na Bernadi Magawa.

Naye kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Honorina Mkunda ameahidi kuhakikisha fedha zote zilizotolewa na serikali zinafanya kazi ilivyokusudiwa ili kuendelea kusogeza huduma kwa wananchi.

Sauti ya kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi .

Katika hatua nyingine katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Bahi Fatuma Sanda akikiwakilisha Chama Cha Mapinduzi, amepongeza juhudi za serikali katika kutekeleza kwa kasi miradi hiyo wilayani Bahi.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wilaya ya Bahi.