Dodoma FM

Wakazi kata Ntyuka kuondokana na adha ya maji

2 June 2023, 1:21 pm

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na viongozi wengine wakizindua mradi huo wa maji. Picha na Seleman Kodima.

Na Selemani Kodima.

Wakazi  4,441 wa mitaa ya Chimalaa na Nyerere   kata ya Ntyuka  jijini Dodoma wanatarajiwa  kuondokana na adha ya kutopata uhakika wa  maji safi na salama  baada ya uzinduzi wa mradi wa maji  wa Ntyuka Chimalaa kukamilika  .

Wakizungumza katika uzinduzi wa mradi huo ambao umetekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA ), baadhi ya wananchi wa kata hiyo wameeleza furaha yao baada ya uzinduzi huo na namna walivyoteseka miaka ya nyuma kutafuta huduma ya maji safi na salama

Sauti za Wananchi.

Katika tukio hilo la uzinduzi wa mradi wa maji ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema uzinduzi wa mradi huo ni hatua kubwa ambayo itasaidia kubadilisha mifumo ya maisha kwa wanajamii wa Ntyuka.

Sauti ya Naibu Waziri wa Maji .
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akimtua mama ndoo kichwani ishara ya kumaliza tatizo la maji katika eneo hilo. Picha na Seleman Kodima.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph, amesema kuwa mradi huo utawanufaisha wakazi zaidi ya 4,441 katika maeneo ya Ntyuka mtaa wa Chimalaa na Nyerere ambao kwa sasa watapata maji kwa asilimia 97 kutoka asilimia 0 ya awali.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majasafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA)
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akifungua akikinga maji bombani baada ya kuzindua mradi huo. Picha na Seleman Kodima.

Naye diwani wa kata ya Ntyuka Yona Andrea amesema kuwa mradi huo wa maji utawanufaisha wakazi wapatao 13,543   ndani ya kata yake huku akimwomba Waziri wa Maji kuwasaidia kupeleka huduma ya maji kwenye zahanati ya Ntyuka .

Sauti ya Diwani wa kata ya Ntyuka.

Imeelezwa kuwa gharama kamili za kutekeleza mradi huo wa maji  wa Ntyuka Chimalaa  ni kiasi cha shilingi milion  471.8 ikiwa ni hatua muhimu ya utatuzi wa adha ya maji kwa wakazi wa jiji la Dodoma.