Dodoma FM

Wakulima wa mtama wanufaika na mbegu za mesia

1 June 2023, 2:14 pm

Shamba la mtama aina ya Mesia katika wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma. Picha na Mindi Joseph.

Mtama ni miongoni mwa mazao ya nafaka yanayolimwa kwa wingi nchini na duniani kote na zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara.

Na Mindi Joseph.

Wakulima wa zao la mtama mkoani Dodoma wamesema mbengu za mtama aina ya mesia zimewanufaisha katika uzalishaji kwani  wameweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wakulima ambao wamesema kuwa uunaji wa zao la mtama umekuwa na tija kwani mbegu hiyo inastahimili ukame.

Sauti za wakulima wa zao la Mtama.
Wakulima wa Mtama aina ya mesia . Picha na Mindi Joseph.

Makamu mwenyekiti wa shirika la uzalishaji mbegu Chamwino DASPA Janeth Nyamayahasi amesema mtama wa mesia unaokoa familia kwani uzalishaji wake hausuisui.

Sauti ya Makamu mwenyekiti wa shirika la Uzalishaji Mbegu Chamwino DASPA