Dodoma FM

Serikali kufanya majaribio ya treni ya mwendokasi Julai

1 June 2023, 1:50 pm

Picha ni aina ya Treni ya mwendo kasi SGR . Picha na Alfred Bulahya.

Hayo yamesemwa na msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Na Alfred Bulahya.

Serikali inatarajia kufanya majaribio ya treni ya mwendokasi (SGR) ifikapo mwezi Julai mwaka huu badala ya mwezi Mei kama ilivyotangazwa hapo awali.

Hayo yamebainisha leo kupitia kwa msemaji mkuu wa serikali Bw. Gerson Msigwa wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma.

Amezitaja sababu zilizokwamisha kuanza kwa majaribio hayo mwezi Mei mwaka huu kuwa kutokana na kuchelewa kwa vichwa vya treni vilivyotarajia kuwasili mwezi April mwaka huu.

Sauti ya Msemaji mkuu wa Serikali.

Aidha akaeleza mwenendo wa ukarabati wa mabehewa mengine yanayotengenezwa nchini Korea.

Sauti ya Msemaji mkuu wa Serikali.
Pia amekanusha taarifa za kukamatwa kwa ndege ya mizigo aina ya Boeing 767-300F kutoka Tanzania . Picha na Alfred Bulahya.

Katika hatua nyingine amekanusha taarifa za kukamatwa kwa ndege ya mizigo aina ya Boeing 767-300F kutoka Tanzania inayodaiwa kukamatwa ikisafirisha mizigo haramu.

Sauti ya Msemaji mkuu wa Serikali.