Dodoma FM

Serikali kuwaunga mkono wajasiriamali wa WAUVI

31 May 2023, 12:37 pm

Wanachama 3000 wa taasisi ya wanawake na uchumi wa viwanda mkoa wa Dodoma, wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali yaliyohusu usindikaji wa vvyakula, matunda na mbogamboga. Picha na Noah Patrick.

Wajasiriamali hao wametakiwa kuacha kutengeneza bidhaa kwa mazoea badala yake wabadilike na kupiga hatua.

Na Alfred Bulahya.

Zaidi ya wanachama 3000 wa taasisi ya wanawake na uchumi wa viwanda mkoa wa Dodoma, wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali yaliyohusu usindikaji wa vyakula, matunda na mbogamboga pamoja na utengenezaji wa sabuni na batiki.

Akifunga mafunzo hayo mapema leo Naibu Waziri wa kilimo na mbunge wa jimbo la Dodoma, Mh Antony Mavunde, akaahidi kuwaunga mkoa wajasiriamali hao kwa kuwahakikishia wanapatiwa mashine za kuchakata bidhaa hizo.

Sauti ya Naibu Waziri wa kilimo na Mbunge wa jimbo la Dodoma

Mbali na hilo akawataka kuacha kutengeneza bidhaa kwa mazoea huku Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara akisema serikali itawaunga mkono wajasiriamali hao katika kuendeleza viwanda watakavyovianzisha.

Sauti ya Naibu katibu mkuu wizara ya uwekezaji viwanda na biashara
Wanachama 3000 wa taasisi ya wanawake na uchumi waviwanda mkoa wa Dodoma, wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali yaliyohusu usindikaji wa vvyakula, matunda na mbogamboga. Picha na Noah Patrick.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mwenyekiti WUVI taifa Habiba Ryengite, ameeleza matarajio ya umoja huo huku mwenyekiti WAUVI mkoawa Dodoma akiomba eneo la kutengeneza viwanda kwani wanachama wapo tayari sasa kuanza uzalishaji.

Sauti ya Mwenyekiti WUVI Taifa .