Dodoma FM

DUWASA kuchimba visima 30 kuanzia Julai

31 May 2023, 5:11 pm

Zoezi la ujenzi wa matenki ya maji katika baadhi ya maeneo linaendelea . Picha na Mindi Joseph.

Hadi kufika mwaka 2051 Duwasa inatarajia kuzalisha lita za maji milion 417 kwa siku.

Na Mindi Joseph.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA)  inatarajia kuchimba visima 30 vya maji katika maeneo yote mkoani Dodoma kuanzia mwezi Julai.

Hayo yamebainsihwa na Mkurugenzi wa huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira Duwasa Mhandisi Emmanuel Mwakabole wakati akizungumza na wanachi wa mtaa wa Mbwanga.

Mkurugenzi wa Huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira Duwasa Mhandisi Emmanuel Mwakabole wakati akizungumza na wanachi wa Mtaa wa Mbwanga.Picha na Mindi Joseph.

Amesema uchimbaji wa Visima Hivyo 30 utasaidia kutatua changamoto ya maji kwa wakazi hao.

Sauti ya Mkurugenzi wa Huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira Duwasa .

Tayari Duwasa imetekeleza Uchimbaji wa visima vya maji katika Eneo la Nzunguni visima 5.

Sauti ya Mkurugenzi wa Huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira Duwasa .