Dodoma FM

Wananchi Bahi Makulu kupelekewa huduma ya maji

29 May 2023, 8:09 pm

Mhe Nollo akiwa na wanakwaya kigango cha Bahi Makulu. Picha na Bernadi Magawa.

Na Bernad Magawa.

Mbunge wa jimbo la Bahi Mheshimiwa Kenneth Nollo ameahidi kupeleka huduma ya maji safi katika kijiji cha Bahi Makulu ili kuwaondolea adha wananchi kutokana na kutokuwepo kwa huduma hiyo kijijini hapo.

Nollo ameyasema hayo Mei 28, 2023 aliposhiriki ibada na kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa Katoliki kigango cha Bahi Makulu ambapo zaidi ya shilingi milioni 5.4 zilichangwa huku Mheshimiwa Nollo akichangia milioni 1.5 kwa ajili ya kuezeka paa la kanisa hilo ambalo boma limejengwa kwa nguvu za waumini ambapo kanisa hilo linatarajia kugharimu zaidi ya shilingi milioni 75 mpaka kukamilika.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Bahi.

Akizungumza katika harambee hiyo, diwani wa kata ya Mpamantwa ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na maji wilaya ya Bahi Mheshimiwa Sostenes Mpandu amemshukuru mbunge kwa utayari wake wa kushiriki katika kazi hiyo ya kiimani.

Sauti ya Sostenes Mpandu.
Mhe. Nollo akizungumza na waumini wa kabisa katoliki kigango Cha Bahi makulu. Picha Bernad Magawa.

 Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Dekania ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji Bwana Alex Madabasi amempongeza Mheshimiwa Nollo kwa kusimamia vema maendeleo ya jimbo la Bahi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Dekania ya Mtakatifu yohane mbatizaji.