Dodoma FM

Wanawake, vijana watakiwa kubadili mitazamo na kushiriki katika sekta ya kilimo

24 May 2023, 7:17 pm

Makamu mwenyekiti kamati ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mh. Mariam Ditopile akizungumza katika mdahalo huo mapema leo hii. Picha na Mariam Kasawa.

Jukumu kubwa la taasisi ya uboreshaji wa mifumo na masoko ya kilimo AMDT ni kuwezesha na kuboresha mabadiliko makubwa ya kimkakati kwenye mifumo ya masoko ya sekta za kilimo.

Na Mindi Joseph.

Vijana na wanawake wametakiwa kubadili mitazamo na kushirikiana na serikali ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika sekta ya kilimo.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na makamu mwenyekiti kamati ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mh. Mariam Ditopile katika mdahalo wa wanawake vijana na uongozi kwenye sekta ya kilimo na biashara.

Amesema vijana na wanawake wana wajibu wa kutumia muda na kuwekeza katika kilimo kwa ufanisi mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi.

Sauti ya Mh Mariam Ditopile.
Baadhi ya washirki walio shiriki katika mdahalo huo kutoka sehemu mbalimbali. Picha na Mariam Kasawa.

Kwa upande wao vijana walioshiriki katika mdahalo huo wamesema uwepo wa wanawake na vijana katika kilimo ni muhimu.

Sauti za vijana washiriki.

Meneja mwandamizi Jinsia, Vijana na Mazingira ya Biashara Mary Kalavo kutoka taasisi ya uboreshaji wa mifumo na masokoya kilimo AMDT amesema mdahalo huo unalenga kuangalia changamoto zinazowakabili wanawake na vijana katika Kilimo.

Sauti ya Bi.Mery Kalavo
Meneja Mwandamizi Jinsia Vijana na Mazingira ya Biashara Mary Kalavo Kutoka Taasisi ya uboreshaji wa mifumo na masokoya kilimo AMDT. Picha na Mariam Kasawa.