Dodoma FM

Fahamu jinsi maziko ya watu wa kale yalivyofanyika

22 May 2023, 4:21 pm

Kaburi la Chifu Masuma Chihoma katika eneo la Iyumbu himaya ya Bwibwi. Picha na George John.

Chifu Chihoma alipata wasaa wa kutuelezea kuhusu uzikaji wa watu wa kale ulivyo kuwa unafanyika.

Na Mariam Kasawa.

Mtazamaji wa Fahari ya Dodoma bado tunaendelea kukujuza mambo mbalimbali hususani historia za kale lengo letu likiwa ni kukuonesha fahari zilizopo hapa mkoani Dodoma.

Mkoa wa Dodoma una historia nyingi za kale ambazo zipo zinazofahamika na zingine zikiwa si maarufu sana .

Kamera ya Fahari imegonga hodi katika himaya ya Bwibwi hapa ni eneo la chifu Lazaro  Chihoma yeye akiwa ametunza mali kale nyingi alizozirithi toka kwa baba na babu zake lakini awali ya yote niliona mawe katika eneo hili nikamuuliza mtemi huyu haya mawe yanamaanisha nini.

Chifu Lazaro Chihoma akizungumza na fahari ya Dodoma nyumbani kwake kabla ya kuelekea katika Himaya ya Bwibwi.Picha na George John.