Dodoma FM

Chamwino watakiwa kukamilisha miradi kwa wakati

19 May 2023, 6:42 pm

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu akizungumza katika ziara wilayani Chamwino.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Katika ziara hiyo ya kikazi katibu Tawala amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Wilaya ya Chamwino, Zahanati ya Kijiji Cha Wilunze na Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya maabara ya kemia na baiolojia katika Shule ya Sekondari Msanga ambavyo ujenzi wake unaendelea.

Na Fred Cheti.

Katibu Tawala mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amewaasa viongozi wa wilaya ya Chamwino kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati pamoja na kuzingatia ubora unaokidhi viwango vinavyotakiwa.

Maagizo hayo yametolewa na Bw. Gugu alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri ya Chamwino na kuongea na watumishi wa wilaya hiyo kwa lengo la kuweka mikakati bora ya utendaji kazi ili kutimiza azma ya maendeleo kwa uharaka.

Sauti ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.

Ujenzi wa jengo la ofisi wilayani Chamwino. Picha na Mkoa wa Dodoma.

Hata hivyo Bw. Gugu amewausia watumishi wa Wilaya hiyo kuwa waadilifu kazini, kudumisha ushirikiano, kuheshimiana bila kujali nyadhifa walizonazo

Sauti ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Utumishi Mkoa wa Dodoma Bi. Coletha Kiwale amepongeza juhudi za mwelekeo wa kumalizika kwa miradi mbalimbali ikiwemo Zahanati ya Kijiji Cha Wilunze ambayo imefikia hatua ya umaziaji.