Dodoma FM

Wenyeviti wa vijiji Bahi watakiwa kuweka wazi mapato na matumizi kwa wananchi

17 May 2023, 12:54 pm

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kata ya Kigwe wakiwa kwenye kikao. Picha na Bernad Magawa.

Viongozi wa eneo hilo pia walilalamika wananchi wao kukosa huduma ya maji safi na salama kwa muda mrefu.

Na Bernad Magawa.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Stuwart Masima amewaagiza wenyeviti wa serikali vijiji wilayani humo kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara ili kuweka uwazi wa fedha za serikali kwa mujibu wa sheria.

Masima ametoa maagizo hayo baada ya kukamilika kwa kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho kata ya Kigwe kilichoketi Mei 16, 2023 ambacho yeye na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya walihudhuria kama sehemu yao ya kutembelea kata mbalimbali.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi .

Akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wa serikali za vijiji wilayani Bahi, mwenyekiti wa kijiji cha Kigwe Jeremia Sobai ameahidi kutekeleza maagizo hayo kikamilifu kwani ni wajibu wao kufanya hivyo.

Sauti ya Jeremia Sobai- Mwenyekiti wa kijiji cha Kigwe.

Katika hatua nyingine Masima alimuagiza kwa njia ya simu Mhandisi wa Ruwasa wilaya ya Bahi kuhakikisha huduma ya maji katika kitongoji cha Kichangani kijiji cha Kigwe inarejeshwa mara moja ili kuwanusuru wananchi wa eneo hilo dhidi ya maradhi ya mlipuko wanayoweza kuyapata kwa kukosa huduma ya maji safi.

Sauti ya Masima akitoa maagizo kuusu huduma ya maji.