Dodoma FM

TMO yawasilisha rasimu ya ujenzi wa kituo cha michezo Mbande

17 May 2023, 4:51 pm

Baadhi ya viongozi wa serikali wilayani Kongwa pamoja na viongozi wa Taasisi hiyo wakifatilia kwa makini rasimu hiyo.Picha na Alfred Bulahya.

Kwa mujibu wa viongozi wa Taasisi hiyo  ujenzi wa Kituo hicho utaleta tija kwa wananchi kwani utahusisha maeneo ya vitega uchumi mbalimbali yakiwemo maduka na huduma nyinginezo.

Na Alfred Bulahya.

Taasisi ya Tembea Kwa Matumaini Organization (TMO) imewasilisha rasimu ya ujenzi wa Kituo cha michezo kinachotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Mbande Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa rasimu  ya awali iliyowasilishwa na msanifu Fadhili Ally Namkumbe  kutoka Place plan Consultant, ujenzi utagharimu takribani shilingi bil 12.

Sauti ya msanifu Fadhili Ally Namkumbe  kutoka Place plan Consultant,

Mkurugenzi Mtendaji Halmahauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary A. Nkullo kwa kushiirikiana na wakuu wa Divisheni na vitengo sanjali na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama, wameridhia mpango huo.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Halmahauri ya Wilaya ya Kongwa .
Msanifu Fadhili Ally Namkumbe  kutoka Place plan Consultant. Picha na Alfred Bulahya.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo (TMO) Bwana Mohamed Hemed, ametoa shukrani za pekee kwa wajumbe wa kikao hicho cha kupitisha rasimu na ameahidi shughuli za ujenzi kuanza mara moja.

Sauti ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo (TMO).