Dodoma FM

NIDA yatoa vitambulisho 62,258 Kongwa

17 May 2023, 3:03 pm

Mkuu wa wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, msajili vitambulisho vya taifa NIDA na viongozi wa Kijiji cha Pingalame. Picha na Benadetha Mwakilabi.

Changamoto wanazopitia wananchi katika vitambulisho vya Taifa ni pamoja na kushindwa kutimiza vigezo na masharti ya kujaza fomu za kuomba vitambulisho hivyo hali inayopelekea ofisi kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) wilaya ya Kongwa imepokea vitambulisho vya Taifa 62,258

Akiongea katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Pingalame kitongoji cha Subugo Afisa usajili wilaya ya Kongwa bwana Said Hamad amesema wamepokea vitambulisho hivyo mwezi Mei ambapo vitambulisho hivyo vitaanza kugawiwa kwa wananchi vijijini muda wowote kuanzia Jumatatu ya tarehe 22 mwezi huu.

Sauti ya Afisa usajili wilaya ya Kongwa .

Aidha Hamad amewasihi wananchi katika Kila Kijiji kufatilia matangazo yatakayotolewa katika maeneo yao juu ya nàmna ya kuchukua vitambulisho hivyo.

Sauti ya Afisa usajili wilaya ya Kongwa .

Hamad ameongeza kuwa kumekuwa na changamoto nyingi wanazokutana nazo katika kuwasajili wananchi katika vitambulisho vya taifa ikiwemo wananchi kushindwa kutimiza vigezo na masharti ya kujaza fomu za kuomba vitambulisho Hali inayopelekea ofisi kushindwa kufanya kazi yake Kwa ufanisi.

Sambamba na hayo Hamad amejibu malalamiko ya hivi karibuni yaliyotolewa na wananchi hususani wa kata ya Kibaigwa juu ya kuchelewa Kwa vitambulisho vya taifa.

Sauti ya Hamad.

Katika maelekezo yake mkuu wa wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel ameagiza wàtendaji wa vijiji kuandaa orodha ya wananchi ambao bado hawajapata vitambulisho na ambao wapo kwenye mchakato ili ofisi ya usajili ishughulikie.

Sauti ya mkuu wa wilaya Kongwa.