Dodoma FM

Wakazi wa Manda watakiwa kushirikiana na walimu

12 May 2023, 3:40 pm

Picha ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Maila Sekondari kwa mwaka 2022/2023 ilishika nafasi ya tatu kwa ngazi ya Wilaya matokeo ya kidato cha nne na nfasi ya pili kwa matokeo ya kidato cha pili.

Na Victor Chigwada.

Afisa elimu wa Kata ya Manda Bw.Christopher Mataya  ametoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano na walimu pamoja na watoto wao ili kuongeza nguvu ya ufaulu katika shule zao

Mataya ameyasema hayo wakati akizungumza na Taswira ya Habari  kuhusu mikakati ya kata yao katika uboreshaji wa elimu ambapo amesema suala la kupata matokeo mazuri ni wajibu wa mzazi kwa ushirikiano na walimu kuanzia ngazi ya msingi mpaka sekondari .

Sauti ya Afisa elimu wa Kata ya Manda

Ameongeza kuwa Maila sekondari wamefanikiwa kupata matokeo mazuri kwa kidato cha nne na cha pili mwaka jana suala lililo chagizwa na fursa ya uwepo wa  mabweni kwa upande wa wasichana kupitia mradi uliofadhiliwa na shirika la Innovation of Africa

Sauti ya Afisa elimu wa Kata ya Manda.

Aidha Mataya amesema  kumekuwa na changamoto ya utoro wa wanafunzi jambo linalo changiwa na baadhi ya wazazi kutokuona umuhimu wa elimu kwa watoto wao.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Manda Bw.Fedrick Mandyamba amewapongeza baadhi ya wazazi kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa walimu na kuhakikisha wanafunzi wanakuwa namatokeo mazuri

Sauti ya Diwani wa kata ya Manda.