Dodoma FM

NEEC na Bodi ya wakala wa uwezeshaji wananchi Zanzibar zasaini mkataba wa ushirikiano

12 May 2023, 1:18 pm

Mtendaji mkuu wa baraza la NEEC Bi Beng’i Issa wakionesha mkataba huo . Picha na Fred Cheti.

Tukio hilo la utiaji Saini limefanyika katika ofisi za baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizopo eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

Na Fred Cheti.

Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) pamoja na Bodi ya wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar zimesaini mkataba wa ushirikiano wa kazi zao za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Tukio hilo la utiaji Saini limefanyika katika ofisi za baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizopo eneo la Nzuguni jijini Dodoma ambapo Mtendaji mkuu wa baraza la NEEC Bi Beng’i Issa anaeleza lengo la makubaliano hayo.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji NEEC
Picha ni Viongozi hao wakiwa wanasaini mkataba wa ushirikiano . Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kutoka Zanzibar Bwana Juma Mohamedi pamoja na Mkurugenzi wa wakala wa Uwezeshaji Bwana Juma Burhan Zanzibar nao wanaelezea jinsi ambavyo ushirikiano huo utakua na tija.

Sauti za Wakurugenzi uwezeshaji Zanzibar.
Mwenyekiti wa bodi ya wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kutoka Zanzibar Bwana Juma Mohamedi. Picha na Fred Cheti.