Dodoma FM

Mndolwa azitaka kampuni zilizoshinda zabuni kufanya upembuzi yakinifu

12 May 2023, 12:42 pm

Baadhi ya wakurugenzi wa makampuni zaidi ya sita , wenyeviti wa vijiji, viongozi wa skimu na wakulima wakiwa katika mkutano huo. Picha na Mindi Joseph.

Hata hivyo Mdolwa amesema lengo la kukutana na wakurugenzi wa kampuni hizo ni kujenga uelewa wa pamoja kurahisisha utendaji na kupata matokeo chanya.

Na Mindi Joseph.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa amezitaka kampuni zilizoshinda zabuni za kufanya upembuzi yakinifu katika mabonde 22 ya kimkakati nchini.

Mdolwa ameyasema hayo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na wakurugenzi wa makampuni zaidi ya sita wakiwemo wenyeviti wa vijiji, viongozi wa skimu na wakulima wa maeneo hayo.

Amewasisitiza wahandisi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji waliopo maeneo yanayotekelezwa zoezi hilo kufanya kazi kwa pamoja na makampuni hayo ili kuhakikisha zoezi hilo linafikia malengo yaliyokusudiwa.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa akizungumza na katika kikao hicho.Picha na Mindi Joseph.

Kwa upande wao Wakurugenzi wa makampuni hayo wamesema wamejipanga kutekeleza zoezi hilo kwa weledi na ufanisi.

Sauti za WAKURUGENZI Boniface Kirigia – Mkurugenzi Royal Associate LTD. 2. Eng. Cyprian Sweke – Mkurugenzi G-PES LTD.