Dodoma FM

Serikali kushirikiana na sekta binafsi kuendeleza sekta ya kilimo

11 May 2023, 5:50 pm

Washiriki katika uzinduzi wa Mradi wa kuimarisha Sekta Binafsi ya Feed the Future Tanzania PSSA. Picha na Mindi Joseph.

Feed the Future inasaidia Nchi katika kuendeleza sekta za kilimo ili kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara ambayo huongeza mapato na kupunguza njaa umaskini na utapiamlo.

Na Mindi Joseph.

Serikali kwa Kushirikiana na Sekta Binafsi imejipanga kuendeleza sekta ya kilimo Kupitia Mradi wa PSSA.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Omar ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika uzinduzi wa Mradi wa kuimarisha Sekta Binafsi ya Feed the Future Tanzania PSSA.

Amesema Tanzania ina vijana takriban milion 16 hivyo kilimo kinasaidia kuchangia katika ajira.

Sauti ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Omar akizungumza katika uzinduzi huo. Picha na Mindi Joseph.

Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani USAID limetoa zaidi ya Dola Milioni 12 ili kuimarisha ujasiri wa vijana katika sekta ya kilimo.

Hii ikiwa ni sehemu ya ni Mpango wa Serikali ya Marekani wa kukabiliana na njaa na usalama wa chakula Duniani kwa kuzingatia wakulima wadogo hasa wanawake

Na Hapa vijana wanasema.

Sauti za Vijana.
Washiriki katika uzinduzi wa Mradi wa kuimarisha Sekta Binafsi ya Feed the Future Tanzania PSSA. Picha na Mindi Joseph.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Katibu tawala Msaidizi Aziza Mumba anasema Mkoa wa Dodoma una hekta zaidi ya Milion 2 kwa ajili ya kilimo huku asilimia 50 tu ndio inatumika katika kilimo.

Sauti ya Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.