Dodoma FM

Wakazi wa Nagulo waiomba Serikali kuwapatia huduma ya umeme

10 May 2023, 7:24 pm

Wakazi hao wanasema kukosekana kwa huduma ya umeme kijijini hapo kunachelewesha maendeleo. Picha na Fahari ya Dodoma.

Hivi karibu Serikali kupitia wizara ya Nishati wanakusudia  kuongeza mafungu katika Mfuko wa Nishati Vijijini ili kuongeza kasi ya kufikisha umeme katika vitongoji 36,336 .

Na Victor Chigwada.

Inaelezwa kuwa nishati ya umeme ni muhimu kwa maendeleo ya jamii ikiwamo kuongeza ufanisi wa huduma za elimu,afya na sekta nyingine hivyo ikikosekana inaweza kuchelewesha maendeleo hususani katika jamii masikini

Hayo yanathibitishwa na wananchi wa kijiji cha Nagulo Kata ya Mpwayungu wakati wakiiomba  Serikali kuwasambazia nishati hiyo katika vitongoji vyao ili kuongeza chachu ya kukuza maendeleo

Sauti ya wananchi wa Nagulo.
Changamoto  hii ya kukosekana kwa nishati ya umeme imekuwa kilio kikubwa hususani kwa wananchi wa vijijini na kusababisha  kudhoofisha ukuaji wa kiuchumi kwa wananchi. Picha na Mindi Joseph.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Meshaki Matonya ametoa wito kwa Serikali kukamilisha  usambazaji wa  umeme katika vitongoji ili kusaidia kurahisisha msukumo wa maisha

Sauti ya Mwenyekiti .

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mpwayungu Bw.Antony Sakalani  amesema kuwa usambazaji wa nishati hiyo ndani ya kata yake ni hafifu kwani umeme uliopo haujawafikia wananchi wengi wa vitongoji vya pembezoni

Sauti ya Diwani

Sakalani ameongeza kuwa bado wanaendelea na jithada za kuwaomba mamlaka husika ya nishati hiyo kuhakisha wanakamilisha usambazaji wa umeme kwa vitongoji vilivyo baki

Sauti ya Diwani.