Dodoma FM

NEMC yatoa mrejesho juu ya kufungia sehemu zenye kelele chafuzi

9 May 2023, 3:11 pm

Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa hiyo hapo jana. Picha na Fred Cheti.

Mnamo tarehe Moja Mei mwaka huu baraza hilo la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilitangaza kuanza opresheni ya kukamata na kufungia maeneo ya kumbi za strehe,nyumba za ibada pamoja na maeneo mengine yanayosababisha mitetemo na kelele kinyume na sheria .

Na Fred Cheti.

Baraza la Taifa la uhifadhi na  Usimamizi wa Mazingira (NEMC) jana limetoa taarifa yake juu ya mrejesho wa operesheni ya kukamata na kufungia maeneo ya starehe na ibada yanayodaiwa kusababisha kelele chafuzi.

Opresheni hiyo imefanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia Mei Mosi mwaka huu hadi Mei 7 ambapo  taarifa hiyo ya mrejesho wa kilichofanyika imetolewa  na  Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Samuel Gwamaka wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Sauti ya Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu NEMC.Picha na Fred Cheti.

Aidha Dkt. Gwamaka amewataka wamiliki wa maeneo yote waliyoyafungia kufuata masharti haya endapo watahitaji kufunguliwa ili waendelea na shughuli zao.

Sauti ya Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo.