Dodoma FM

Wawekezaji watakiwa kufanya tahmini ya athari za mazingira

5 May 2023, 2:45 pm

Bwn. Abel Sembeka Meneja wa tathmini ya athari za Mazingira NEMC. Picha na Fred Cheti.

Na Fred Cheti.

Baraza la Usimamizi na uhifadhi wa Mazingira (NEMC) limewataka wawekezaji wote  wa miradi ya maendeleo nchini kufanya tathimini ya athari kwa mazingira katika miradi yao ili kuepusha migogoro itakayotokana na uchafuzi wa mazingira.

Hayo yameelezwa na Bwn. Abel Sembeka Meneja wa tathmini ya athari za Mazingira katika baraza hilo ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu kwa wawekezaji wa miradi mbalimbali juu ya umuhimu wa kufanya tathmini hiyo ya athari kwa mazingira (TAM)

Sauti ya Meneja tathmini athari za mazingira.
Ujenzi ni moja ya shughuli zinazo fanywa na wawekezaji katika mazingira. Picha na Fred Cheti.

Bwana Sembeka amesema serikali kupitia baraza hilo itaendelea kutoa elimu kwa wawekezaji wote kuhusu suala la utunzaji wa mazingira ili ukuaji wa uchumi nchini unaochangiwa na wawekezaji uende sambamba na utunzaji wa mazingira.