Dodoma FM

Wafanyabishara Maisha plus waiomba serikali kufanya ukarabati

5 May 2023, 4:38 pm

Muonekano wa Mabanda ya kuuzia Samaki katika Soko la Maisha plus. Picha na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara wanasema kuwa  viongozi hao wamekuwa wakiahidi kupatia ufumbuzi baadhi ya changamoto hizo bila ya kutekeleza ahadi hizo.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara wa matunda na mbogamboga  katika soko la maisha plus jijini Dodoma wameiomba serikali kufanya marekebisho kwa haraka kwani ni muda mrefu umepita tangu kuahidiwa ujenzi huo.

Dodoma Tv imefika katika soko hilo na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara ambapo wamesema kuwa ni zaidi ya miaka mitatu imepita tangu serikali kubomoa baadhi ya vibanda kwa ajili ya marekebisho lakini bado suala hilo halijafanyiwa kazi.

Sauti za wafanyabiashara.
Muonekano wa baadhi ya mabanda katika soko la Maisha plus .Picha na Thadei Tesha.

lakini je ni kwa kiasi gani wanaathirika kutokana na chanagamoto hiyo?

Sauti za wafanyabiashara.