Dodoma FM

Mila na desturi kandamizi zatajwa kumdidimiza mwanamke

5 May 2023, 3:06 pm

Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia kutoka Taasisi iyokuwa ya kiserikali ya Action for community care Bi Stella Matem. Picha na Alfred Bulahya.

Aidha ameisihi jamii kuwaamini wanawake katika maamuzi kwani hata Dira ya Taifa ya 2025 ya JMT,  Malengo ya Maendeleo Endelevu (2030) hasa lengo Na. 5 na MKUKUTA (I&II) vinataka kuwepo kwa usawa katika masuala ya uongozi ama maamuzi. 

Na Alfred Bulahya.

Mila na desturi kandamizi zimetajwa kuwa bado ni sababu zinazomkandamiza mwanamke kushiriki maamuzi katika ngazi ya familia hali inayoendelea kumdidimiza mwanamke.

Hayo yamebainishwa na Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia kutoka Taasisi iyokuwa ya kiserikali ya Action for community care Bi Stella Matem, wakati akizungumza na Dodoma tv.

Amesema Pamoja na kwamba wanawake ni wengi zaidi ya nusu ya watu wote nchini kwa mujibu wa SENSA ya watu na makazi ya 2022, bado idadi yao katika vyombo vya maamuzi ni ndogo.

Sauti ya Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia.