Dodoma FM

Mchezo wa kriketi kuongeza mahudhurio ya wanafunzi

4 May 2023, 1:03 pm

Walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani Kongwa walio kuwa wakipatiwa mafunzo ya kriket katika shule ya msingi Viganga wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Benadetha Mwakilabi.

Afisa michezo wilayani Kongwa  amesema wanawajengea uwezo walimu waweze kuwasaidia watoto kumudu vitendo vya mchezo wa kriketi ili kupitia ubora wa timu za shule zao waweze kupata wachezaji wazuri wa kuunda timu za Wilaya  na pia wapate fursa ya kuchaguliwa kujiunga na timu za Taifa za miaka 15, 17, 19 kwa upande wa wasichana na wavulana.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Walimu wahitimu wa mafunzo ya mchezo wa Kriketi wilayani Kongwa wamesema uwepo wa mchezo huo mashuleni unasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza adha ya utoro mashuleni kwani watoto wengi wanavutiwa kucheza na kushiriki tangu ulipoletwa wilayani humo mwaka 2021.

Walimu hao wameeleza hayo wakati wa kufunga mafunzo ya Kriketi kwa walimu wa shule 12 za msingi na sekondari za kata ya Kongwa yaliyofanyika katika kituo cha shule ya msingi Viganga ambapo wameshukuru pia chama Cha Kriketi Taifa (TCA) kwa kuleta mafunzo hayo.

Sauti ya GINETHON NDUNGURU wa shule ya sekondari Kongwa
Sauti ya REHEMA MOSHI MAGOME  wa shule ya msingi Mlanga
Mwanafunzi akiwa katika mazoezi ya Mchezo huo wa Kriketi . Picha Benadetha Mwakilabi.

Kwa upande wake mratibu wa Kriketi wilaya Kongwa Bwana Khassim Nassoro amewasihi walimu hao kuyashika yote waliyofundishwa kwa vitendo na kwenda kuwapatia ujuzi huo wanafunzi mashuleni ili kuzalisha wachezaji mahiri wa Kitaita na kimataifa wa mchezo huo.

Sauti ya KHASSIM NASSORO mratibu wa Kriketi Kongwa.
Sauti ya KHASSIM NASSORO mratibu wa Kriketi Kongwa
Walimu wakiwa katika mafunzo ya mchezo huo . Picha na Benadetha Mwakilabi.

Aidha Kwa upande wake Afisa michezo wilaya Kongwa Bwana Kelvin Msumule amesema baada ya mafunzo hayo wanatarajia kufanya mafunzo kama haya katika kituo cha shule ya Pandambili.

Sauti ya KELVIN MSUMULE Afisa michezo wilaya Kongwa.