Dodoma FM

Wananchi Ng’ambi watakiwa kutunza mazingira

3 May 2023, 1:59 pm

Mradi wa kisasa wa ufugaji nyuki katika kijiji cha Ng’ambi walayani Mpwapwa.Picha na Fred Cheti.

Amesema mazingira yakitunzwa vema yanaweza kutengeneza fursa mbalimbali kwa wananchi.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe. Sophia Kizigo amewataka wananchi wa kijiji cha Ng’hambi wilaya humo kuwa mabalozi wa utunzaji wa mazingira illi kutengeneza fursa nyingi za ajira zinazotokana na utunzaji wa mazingira.

Mhe. kizigo ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachi wa kijiji cha Ng’ambi wilayani humo baaada ya kufungua mafunzo ya ufugaji nyuki wa kisasa kwa wanakikundi 80 katika kijiji hicho chini ya Mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia mifumo ikolojia vijijini (EBARR).

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mh. Sophia Kizigo akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo. Picha na Fred Cheti.

Aidha Mh. Kizigo ameawataka wananchi hao kutumia mradi vizuri kama sehemu ya ajira ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuleta maendelea katika kijiji hicho.