Dodoma FM

Wafanyabiashara watakiwa kutunza mazingira

2 May 2023, 1:23 pm

Bi Sauda  Mwidusi Kutoka baraza la uhifadhi wa mazingira NEMC. Picha na Thadei Tesha.

Mifuko ya plastiki ilipigwa marufuku kutumika hapa chini hii ni kutokana na wataalamu mbalimbali wa maingira kubainisha kuwa matumizi ya mifuko hiyo huongoza katika suala la uchafuzi wa mazingira.

Na Thadei Tesha.

Wafanyabiashara jijini Dodoma wametakiwa kuendelea kutunza mazingira kwa kuepuka kutumia vifungashio vya plastiki ambavyo ni hatari kwani inaongeza kasi ya uchafuzi wa mazingira.

Hayo yamesemwa na Bi Sauda  Mwidusi Kutoka baraza la uhifadhi wa mazingira NEMC wakati akiungumza na wafanyabiashara katika soko kuu la majengo ambapo amesema ni marufuku kwa mfanyabiashara yoyote kutumia vifungashio vya plastiki kwani ni hatarishi kwa mazingira

Sauti ya Bi Sauda  Mwidusi.
Muonekano wa mazingira ya soko la Majengo kwa nje. Picha na Thadei Tesha.

Aidha ametumia fursa hiyo kubainisha mifuko ambayo imeruhusiwa na seriakli ambayo ni rafiki ya mazingira ambapo pia ameongeza kuwa wanaendelea na kampeni ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki katika masoko yote kwa nchi nzima.

Sauti ya Bi Sauda  Mwidusi.