Dodoma FM

Watanzania wahimizwa kutumia mbolea isiyo zeesha ardhi

1 May 2023, 1:08 pm

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri akizungumza na wananchi alipotembelea kiwanda hicho . Picha na Fred Cheti.

Mbolea inayo zalishwa katika kiwanda hiki cha Intracom kinachopatikana katika kata ya Nala jijini Dodoma inatengenezwa kwa samadi za wanyama na haizeesha ardhi. 

Na Fred Cheti

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabair Shekimweri amewataka wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla kutumia mbolea inayozalishwa katika kiwanda cha Intracom ambayo inatengenezwa kwa samadi za wanyama na isiyozeesha ardhi. 

Mh Jabir ametoa wito huo wakati wa kukabidhi eneo kwa ajili ya ujenzi kituo cha Polisi katika Mradi  wa kiwanda cha Mbolea cha Intracom katika eneo la Nala jijini Dodoma Mradi ambao unatarajia kuzalisha mbolea itakayotumika nchini na nyingine kuuzwa nje ya nchi.

Sauti ya Mkuu wa wialaya ya Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Nduwimana Nazaire.Picha na Fred Cheti.

Aidha Mh. Shekimweri amesem a serikali ya mkoa wa Dodoma ipo katika mchakato wa kupeleka miundombinu mingine mbalimbali ikiwemo barabara na maji  katika sehemu hiyo ambapo kiwanda hicho kinajengwa.

Sauti ya Mkuu wa wialaya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Nduwimana Nazaire nae alikua na haya ya kuzungumza kuhusu mradi huo uatakavyokua na manufaa nchini.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda.