Dodoma FM

Wakulima wa Alizeti walalamika uzalishaji hafifu

1 May 2023, 4:53 pm

Shamba la Alizeti katika kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino. Picha na Mindi Joseph.

Katika mwaka 2019/2020 uzalishaji wa alizeti nchini umefikia tani 649,437 ikilinganishwa na tani 561,297 kwa mwaka 2018/2019.

Na Mindi Joseph.

Wakati Mkoa wa Dodoma ukitegemewa zaidi katika uzalishaji wa mafuta ya alizeti wakulima wamesema mwaka huu uzalishaji wao ni hafifu.

Taswira ya habari imefika katika kijiji cha Makag’wa na kuzungumza na wakulima na hapa wanasema jua na mvua kusuasua ni changamoto inayowakabili katika uzalishaji wa zao hilo.

Sauti za wakulima.

Diwani wa kata ya makag’wa Solomoni Samwel anasema wakulima wengi wamejikita kulima zao la alizeti ili kujikwamua kiuchumi lakini hali ni mbaya mwaka huu.

Sauti ya Diwani.