Dodoma FM

Serikali kuboresha Ranchi ili kupanua soko nje ya nchi

1 May 2023, 3:45 pm

Mheshimiwa Abdalah Ulega akikagua ng’ombe walionunuliwa kutoka nchi za Uganda na Rwanda katika ranchi ya NARCO Kongwa. Picha na Hamashauri ya Kongwa.

Akisoma taarifa meneja wa Ranchi ya Kongwa bwana Elisa Binamungu amesema shilingi bilioni 4.65 zilitengwa Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kuboresha ranchi hiyo ikiwa ni pamoja na kutengeneza Barabara, kuondoa vichaka hekari 8000 kwaajili ya kustawisha mifugo.

NA Bernadetha Mwakilabi.

Waziri wa mifugo na uvuvi Mheshimiwa Abdalah Hamis Ulega amesema kuwa Serikali chini ya wizara yake inaendelea kuboresha ranchi zote ikiwemo ya Kongwa Kwa kununua na kunenepesha ng’ombe, kuboresha miundombinu na kununua vifaa vya kisasa vya kuchakata malisho ya mifugo.

Ulega ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Kongwa alipotembelea Ranchi ya Taifa ya wilayani humo ili kuzindua vifaa vya kisasa vya kuchakata malisho matrekta manne, kuzindua uvunaji nyasi na kukagua ng’ombe walionunuliwa kutoka nchi za Uganda na Rwanda ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi CCM katika wizara ya mifugo na uvuvi.

Sauti ya Waziri wa mifugo.

Pia Ulega ameongeza kuwa Ranchi zinatakiwa kuzalisha majani mengi kwaajili ya malisho ya mifugo yake na kuuza Kwa wananchi ambao ni wafugaji

Sauti ya Waziri wa Mifugo.
Matrekta ya kisasa ya kuchakata malisho ya mifugo yaliyozinduliwa na kuanza matumizi yake. Picha na halmashauri ya wilaya ya Kongwa.

Nae Mwenyekiti wa CCM wilaya Kongwa Mheshimiwa Musa Abdi amemuomba waziri Ulega kuwasaidia kupata mnada wa mifugo katika eneo la mbande ambapo ng’ombe watauzwa Kwa kilo ili kuongeza thamani na kumnufaisha mfugaji.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM wilaya Kongwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambae pia ni mkuu wa wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema ameshauri kuwepo kwa kiwanda Cha maziwa, bucha nje ya Ranchi ya Kongwa ambapo itaongeza utalii na kukuza uchumi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa.