Dodoma FM

Madiwani waomba umeme katika Vitongoji

1 May 2023, 2:49 pm

Madiwani wa wilaya ya Kongwa wakiwa katika kikao. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Mrindoko amesema kutakuwa na SWITCHING STATION eneo la mbande itakayosaidia upatikanaji wa umeme pale inapotokea tatizo eneo Moja lisilete ukosefu wa umeme eneo lingine.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Waheshimiwa madiwani ambao ni wawakikishi wa wananchi  wameomba huduma ya umeme kwenye vitongoji wanavyosimamia Kwani Kuna vitongoji havijapata huduma hiyo mpaka Sasa.

Wakipokea taarifa za taasisi mbalimbali madiwani wa wilaya ya Kongwa wametoa rai yao Kwa kaimu meneja TANESCO wilaya Kongwa kuwasaidia kufikisha umeme katika vitongoji na kuangalia namna ya kufanya Kwa maeneo yenye umeme mdogo ili kuwasaidia wananchi kupata huduma za kusaga karibu na maeneo yao.

Sauti ya Diwani Kata ya Zoissa Mheshimiwa Abdalah Chidundo
Sauti ya Diwani kata ya Matongoro Jeremiah Makanda
Picha ni Madiwani wa wialaya ya Kongwa wakiwa katika kikao pamoja na mkuu wa wialaya ya Kongwa. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Akijibu maswali hayo kaimu meneja wa TANESCO wilaya Kongwa bwana Musa Mrindoko amesema kuwa ofisi imepokea na kuahidi kufanyia kazi suala la upatikanaji wa umeme vitongojini Kwa awamu ya pili Kwani awamu ya kwànza ililenga kuvifikia vijiji ambapo walifànikiwa Kwa asilimia 100.

Sauti ya kaimu meneja TANESCO

Aidha Mrindoko ametoa rai kwa waheshimiwa madiwani kuongea na wananchi juu ya kuto haribu miundombinu ya umeme  Kwani wanaweza kusababisha madhara ya ajali vifo na kukosa huduma ya umeme.

Sauti ya kaimu meneja TANESCO