Dodoma FM

Wahitimu wa mafunzo SIDO watakiwa kuzalisha bidhaa bora

25 April 2023, 12:43 pm

Zaidi ya wahitimu 350 wa mafunzo ya usindikaji wa Vyakula na matunda wakiwa katika kuhitimisha mafunzo hayo. Picha na Alfred Bulahya.

Awali kulitanguliwa na mafunzo y utengenezaji Sabuni na Batiki kama anavyobainisha Mkufunzi wa mafunzo hayo.

Na Alfred Bulahya.

Zaidi ya wahitimu 350 wa mafunzo ya usindikaji wa Vyakula na matunda wamehitimu mafunzo hayo yanayotolewa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO huku wakitakiwa kuhakikisha wanakwenda kutengeneza bidhaa bora.

Mafunzo hayo yaliyodumu kwa kipindi cha Siku Nne yamehusisha wanachaama kutoka Taasisi ya Wanawake na Uchumi wa Viwanda WAUVI ambao wamepata elimu ya namna ya kusindika vyakula mbalimbali na matunda.

Akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa SIDO mkoa wa Dodoma  bw, Twaha Swed amesema wahitimu hao wanatarajia kupatiwa Mashine mbalimbali ili kuanza kufanya kazi.

Sauti ya Meneja wa SIDO mkoa wa Dodoma 

 

Baadhi ya bidhaa hizo zilizo tengenezwa na kuhifadhiwa tayari. Picha na Alfred Bulahya.

Akijibu Risala ya WAUVI Mgeni Rasmi Bi Fatma Toufiq ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge, ya masuala ya ustawi na maendeleo ya jamii ambaye pia ni mbunge Viti maalumu mkoa wa Dodoma, amesema atawasilisha ombi lao kwa Mkurugenzi wa jiji, la kupatiwa eneo la kujenga kiwanda kikubwa.

Sauti ya Bi Fatma Toufiq

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAUVI mkoa wa Dodoma akamuomba mgeni rasim kusaidia upatikanaji wa mikopo huku baadhi ya wahitimu wakiomba mikopo hiyo itolewe kwa wakati.

Sauti ya Mwenyekiti wa Taasisi ya WAUVI