Dodoma FM

Wafanyabishara walia na bei ya viazi mbatata

25 April 2023, 2:23 pm

Mfanyabiashara akipanga viazi katika ndoo kwaajili ya kuviuza . Picha na Thadey Tesha.

Kwa sasa wastani wa bei ya viazi mbatata ni kati ya shilingi 90000 kutoka wastani wa shilingi 60000-70000 kwa gunia.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko kuu la majengo jijini Dodoma wameelezea namna wanavyoathirika kutokana na kupanda kwa bei ya viazi mbatata.

Dodoma Tv imewatembelea Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la majengo jijini hapa ambapo wanasema kuwa kwa sasa bei ya bidhaa ya viazi mbatata imepanda gafla kutokana na changamoto za shambani pamoja na usafirishaji.

Sauti za wafanyabishara.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara pamoja na wananchi jijini hapa wanasema kuwa kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kumeendelea kuwaathiri kutokana na wengi wao kutokuwa na kipato cha kutosha.

Sauti za wafanyabishara.