Dodoma FM

Tume ya Taifa ya umwagiliaji kukarabati skimu za umwagiliaji

25 April 2023, 6:07 pm

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji Raymond Mndolwa akiteta jambo na viongozi wengine wakati mkutano huo ukiendelea. Picha na Fred Cheti.

Mwezi wa tano Tume ya taifa ya umwagiliaji  inatarajia kutia saini mikataba 8 yenye zaidi ya thamani ya zaidi ya shilingi Bilion 59.

Na Mindi Joseph.

Tume ya Taifa ya umwagiliaji leo imetia saini mikataba 4 ya ujenzi na ukarabati wa skimu za umwagiliaji yenye thamani ya zaidi ya Bilion 41.

Akizungumza katika Hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji Raymond Mndolwa amesema Miradi hiyo inalenga kuleta tija na uzalishaji mkubwa kwa wakulima.

Ameongeza kuwa Tangu kuanza kwa bajeti ya mwaka 2022/2023 Tume ya taifa ya umwagiliaji imetia saini Zaidi ya miradi 75 ambayo wakandarasi wapo katika maeno yao ya kazi wakiendelea na utekelezaji.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika hafla hiyo . Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge ambapo miradi hii itatekelezwa wamesema Kilimo cha umwagiliaji kina tija kubwa katika uzalishaji kwa wakulima.

Sauti za wabunge.