Dodoma FM

Mzogole waishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa daraja

25 April 2023, 1:36 pm

Daraja linalojengwa kuunganisha Kijiji Cha Mzogole na Mpinga . Picha na Bernad Magawa.

Ujenzi wa daraja hilo unafuatia baada ya  kujengewa shule kubwa ya Sekondari iliyopo makao makuu ya kata, adha zilizowasumbua wananchi hao tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi.

Na Bernad Magawa.

Wananchi wa kijiji cha Mzogole kata ya Mpinga wilayani Bahi wameishukuru serikali kwa kuanza kuwajengea Daraja litakalounganisha kijiji hicho na makao makuu ya kata .

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara alioufanya Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo katika kijiji cha Mzogole, Diwani wa kata ya Mpinga Kudagana Ndalu pamoja na wananchi wameelezea furaha yao kwa kupatiwa miradi hiyo.

Sauti ya Mhe. Kudagana Ndalu –

Diwani wa kata ya Mpinga Daraja hilo ambalo litagharimu zaidi ya milioni 500 litakapokamilika linaelezwa kutatua changaoto nyingi zilizowasumbua wananchi wa eneo hilo likiwemo la wanafunzi wa sekondari kushindwa kuvuka kwenda shule pindi mto unapojaa.

Sauti ya Silvesta Mlewa – Mwananchi.

Naye mbunge wa Jimbo la Bahi akizungumza na wananchi katika mkutano huo ameeleza namna anavyoendelea kushughulikia Changamoto za kata hiyo ambayo ilikuwa kama kisiwa na kuwataka wananchi kuendelea kuiamini serikali ya awamu ya sita.

Sauti ya Mhe Nollo – Mbunge Jimbo la Bahi.