Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutambua kilimo cha umwagiliaji ni cha uhakika

24 April 2023, 4:04 pm

Wakazi wa Kijiji cha Kongogo wakiwa kwenye mkutano . Picha na Mindi Joseph.

Dodoma ni miongoni mwa mikoa iliyo na hali ya ukame na Hupata wastani hali inayopelekea kulima mazao yanayostahili ukame kama vile uwele, mtama, mahindi, karanga, alizeti, ufuta na zabibu.

Na Mindi Joseph.

Wananchi Kata ya Babayu wamehimizwa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji ambacho uzalishaji wake ni wa uhakika.

Taswira ya habari imezungmza na Mwenyekiti wa kijiji cha Kogongo Daudi Mohamed ambapo amesema serikali inafanya jitihada kubwa za kuboresha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji hivyo ni wakati wa wakulima kujikita katika kilimo hicho kutokana na Mvua kusuasua.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Kogongo Daudi Mohamed.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kogongo Daudi Mohamed akizungumza katika mkutano huo. Picha na Mindi Joseph.

Katika hatua nyingine amesema mashamba ya wakulima yataongezewa thamani kupitia kilimo cha umwagiliaji.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Kogongo Daudi Mohamed.