Dodoma FM

Wananchi Bahi watarajia kuchangia Zaidi ya madawati 10,000

24 April 2023, 2:56 pm

Picha ikionesha mfano wa madawati yatakayo changiwa na wananchi kwaajili ya shule za Msingi na Sekondari wilayani humo.

Pamoja na wilaya ya Bahi kuwa na mafanikio makubwa kitaaluma katika mkoa na taifa, tatizo la kukosekana kwa madawati lisipodhibitiwa linaweza kuwa chanzo cha kupotea kwa mafanikio hayo.

Na. Bernad Magawa.

Wananchi wilayani Bahi wanatarajia kuchangia zaidi ya Madawati elfu 10 kwa shule za Msingi na Sekondari kama sehemu ya wao kuunga mkono juhudi za serikali katika kutoa elimu bure.

Akizungumza katika kikao kilichowahusisha Wanasiasa kutoka kata zote wilaya ya Bahi pamoja na wakuu wa idara na taasisi mbalimbali za Serikali wilayani humo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendeji wa halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji wilaya ya Bahi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mpamantwa Sostenes Mpandu ameeleza namna tatizo la madawati lilivyo kubwa katika wilaya hiyo.

Sauti ya Sostenes Mpandu

Mpandu amesema pamoja na wilaya ya Bahi kuwa na mafanikio makubwa kitaaluma katika mkoa na taifa, tatizo la kukosekana kwa madawati mashuleni lisipodhibitiwa linaweza kuwa chanzo cha kupotea kwa mafanikio hayo.

Hoja hii ikaungwa mkono kikamilifu na viongozi wa Chama na Serikali, hatimaye wote wakatoka na tamko moja la wananchi kushiriki uchangiaji wa madawati ili kukabiliana na kadhia hiyo kama mchango wao katika kuunga mkono juhudi za Serikali ambayo imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye miundombinu ya elimu wilayani Bahi.

Sauti za Viongozi wa Chama na Serikali.