Dodoma FM

Waislamu watakiwa kusheherekea sikukuu kwa amani na upendo

21 April 2023, 1:40 pm

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu. Picha na Fred Cheti.

Waislamu Duniani Kote wanatarajia kusheherekea sikukuu ya EID siku ya kesho siku ya jumamosi .

Na Fred Cheti.

Kuelekea sikukuu ya Eid El Fitr wito umetolewa kwa waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wananchi wote Mkoani Dodoma kusheherekea siku kuu hiyo kwa amani na upendo bila uvunjifu wowote wa amani.

Wito huo umetolewa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu wakati akifanya mahojiano na Dodoma Tv ofisini kwake katika msikiti wa Gaddafi uliopo jijini Dodoma.

Sauti ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Aidha Sheikh Mustafa amewataka waislamu kuyakumbuka makundi mbalimbali yenye uhitaji wakiwemo wajane na masikini katika sikukuu hiyo huku akitoa wito pia kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia sheria barabarani.

Sauti ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma