Dodoma FM

Serikali yajenga nyumba bora za walimu Bahi

21 April 2023, 2:37 pm

Nyumba ya Mwalimu Lukali shule ya Masingi. Picha na Bernad Magawa.

Katika hatua nyingine kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ilibaini Mapungufu katika ujenzi wa vyumba viwili vya Maabara shule ya sekondari Chonama.

Na. Bernad Magwa.

Walimu wa shule za msingi wilayani Bahi wameishukuru serikali kwa kuwajengea nyumba bora za makazi ambazo zimesaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa makazi ya walimu vijijini.

Hayo yamesemwa na Mwalimu makuu wa Shule ya msingi Lukali Tabu Abdalah pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mgondo Ada kahemela walipotembelewa na kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani katika shule hizo.

Wamesema uwepo wa nyumba bora za kuishi ni motisha kwa walimu kwani kumekuwa na changamoto ya makazi ya walimu katika shule hizo zilizosababisha baadhi yao kutowajibika kikamilifu kwani walilazimika kuishi mbali na eneo la kazi.

Sauti za walimu msingi

Katika hatua nyingine kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ilibaini Mapungufu katika ujenzi wa vyumba viwili vya Maabara shule ya sekondari Chonama baada ya shilingi Milioni sitini zilizopelekwa na serikali kuisha bila kukamilisha ujenzi.

Hali hiyo ilimlazimu wenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi Donard Mejiti (MNEC) kutoa maagizo mazito huku akiwaelimisha vibarua katika ujenzi huo kujiendeleza kielimu mara chuo cha VETA Bahi kitakapofunguliwa.

Sauti ya Donalda Mejiti.
Nyumba ya Mwalimu shule ya Msingi Mgondo.Picha Bernad Magawa.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Chonama Dotto Mjezwa alisema shule ilipokea shilingi Milioni sitini kutoka serikalini ambayo tayari imekwisha tumika na inahitajika walau shilingi million sita ili kukamilisha mradi huo.

Sauti ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Chonama.