Dodoma FM

Taasisi na vituo vinavyo hudumia watu wengi kupigwa marufuku kutumia mkaa na kuni

20 April 2023, 11:05 am

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Suleimani Jafo. Picha na Fred Cheti.

Watu wengi hutumia nishati hiyo kwa sababu ni rahisi kupatikana na wanaweza kumudu gharama yake tofauti na nishati nyingine kama umeme na gesi.

Na Fred Cheti.

Inaelezwa kuwa zaidi ya  hekta 46,960 za misitu huharibiwa kila mwaka nchini kwa ajili ya kutengenezea kuni na mkaa, jambo ambalo linaweza kuifanya nchi kuwa jangwa iwapo hatua hazitachukuliwa hatua ili kuzuia hali hii.

Kufuatia hali hiyo Serikali imetangaza kwamba Januari 31, 2024 itakuwa siku ya mwisho kwa taasisi pamoj na vituo vyote vinavyohudumia watu zaidi 100 kutumia Nishati hizo ili kuokoa mazingira dhidi ya ukataji miti zaidi.

Ili kuunga Mkono Juhudi hizo za serikali Dodoma Tv imezungumza na baadhi ya wananchi jijini Dodoma ili kuhoji nini kinasababisha wananchi pamoja na baadhi ya taasisi kuendelea na matumizi ya kuni na mkaa licha ya nishati hizo kutajwa kuwa si rafiki kwa mazingira na nini kifanyike ili kuondoa changamoto hiyo?

Sauti za wananchi
Matumizi ya mkaa na kuni katika jamii ni makuba kwani wananchi wanadai nishati hizi ni rahisi kupatikana .Picha Fred Cheti.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Suleimani Jafo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma  alitangaza kuwa  vituo vyote vinavyohudumia wanaozidi 100 vitatakiwa kuacha kutumia kuni au mkaa ifikapo Januari 31, 2024.

Sauti ya Mh. Suleiman Jafo.

Licha ya sifa yake ya kupatikana kwa urahisi na watu kumudu gharama zake, mkaa na kuni zinatajwa kuwa hatari kwa mazingira.