Dodoma FM

Walimu watakiwa kuzuia maudhui yasiyofaa

13 April 2023, 5:08 pm

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri akiwa shule ya Miyuji sekondari . Picha na Mindi Joseph.

Jiji la Dodoma limetakiwa kutenga fedha na kuongeza vifaa vya Tehama kwa shule kwa lengo la kuendelea kuboresha ujifunzaji wa wanafunzi shuleni.

Na Mindi Joseph.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri amewataka walimu wanaosimamia Tehama kufuatilia kwa karibu maudhui yanayowekwa kwenye vishikwambi na kuzuia maudhui yasiyofaa kwa wanafunzi.

Ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma katika uzinduzi wa Mradi wa kukabidhi vifaa vya tehema uliofanyika katika shule ya Miyuji sekondari vifaa hivyo vitumike kwa malengo yaliyokisudiwa na viwe na usimamizi unaostahili.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri
Wanafunzi wa shule ya Miyuji sekondari wakitazama vifaa hivyo.Picha na Mindi Joseph

Kwa upande wake Mkurugenzi African Child Projects mradi wa kuunganisha shule na internet  Catherine Kimambo amesema milion 48 zimetumika katika shule tisa za Dodoma.

Sauti ya Mkurugenzi African Child Projects

Naye Mkuu wa kanda ya kati Voodacom Joseph Sayi amebainisha kuwa wanafunzi laki 6 wamenufaika na mpango wa uunganishaji wa mtandao nchini.

Sauti ya Mkuu wa kanda ya kati Voodacom Joseph Sayi