Dodoma FM

Waziri Simbachawene azindua mpango mkakati wa mwaka 2022-2027

7 April 2023, 4:59 pm

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene. Picha na Pius Jayunga.

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ameeleza kwamba Mkakati huo utawezesha nchi kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 ambayo yamejikita katika kupunguza umasikini na kuleta ustawi wa maisha ya watu.

Na Pius Jayunga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amezinduaMpango Mkakati wa mwaka 2022-2027 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, Mhe. Simbachawene amesema Mpango Mkakati huo unaotarajiwa kutumia Dola za Marekani milioni  363  unalenga  kuboresha masuala mbalimbali yakiwemo kuimarisha utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na maafa kabla hayajatokea.

Sauti ya Mhe. Simbachawene
Baadhi ya wajumbe walio hudhuria mkutano huo. Picha na Pius Jayunga.

Vile vile amezitaka Wizara, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zitakazonufaika na utekelezaji wa Mkakati huo kushirikiana WFP ili kuhakikisha shughuli zilizopangwa zinatekelezwa na kuchangia katika kuboresha hali za maisha ya watu.

Sauti ya Sauti ya Mhe. Simbachawene

Aidha Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gordon-Gibson ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa usaidizi, uaminifu na ushirikiano wake huku akiahidi kuwa WFP itahakikisha Tanzania inakuwa  nchi endelevu na yenye uwezo wa kustahimili maisha bora kwa Watanzania wote.