Dodoma FM

Dawa zilizo kwisha muda wa matumizi zatajwa kuisababishia Serikali hasara.

7 April 2023, 2:37 pm

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere.Picha na Alfred Bulahya.

Amezitaja baadhi ya hospitali hizo huku akisema dawa hizo zilizoisha muda wake zimekuwepo kwa wastani wa miezi 2 hadi miaka 10.

Na Alfred Bulahya

Kuwepo kwa dawa zilizokwisha muda wa matumizi yake kwenye baadhi ya hospital, vituo vya afya na zahanati, umetajwa kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Bilion 3.5 hali ambayo inaleta hatari iwapo zitatumiwa na binadamu.

Hayo yamebainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere wakati akisoma ripoti ya mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma.

Sauti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia kwa makini mkutano huo wa CAG. Picha na Alfred Bulahya.

Halima Mdee ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC)amesema baadhi ya watendaji wa serikali wamekuwa wakifanya ubadhirifu huo kwa makusudi huku Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mwenyekiti Mhe.Naghenjwa Kaboyoka akawa na haya ya kuzungumza

Sauti za mwenyekiti (LAAC)na Mwenyekiti (PAC)