Dodoma FM

Wawekezaji Mundemu wapewa siku 45 kudhibiti vumbi

6 April 2023, 5:21 pm

Uchimbaji wa kokoto ukiwa unaendelea katika eneo hilo la Mundemu Wilayani Bahi. Picha na Fred Cheti.

Hivi karibuni Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)- Kanda ya Kati kwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi – Dodoma na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi ilifanya Ukaguzi katika eneo la mradi huo.

Na Fred Cheti.                                

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa siku 45 kwa wawekezaji wa mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kudhibiti vumbi linalosambaa na kusababisha kero kwa wananchi.

Pia ametoa muda huo kwa wawekezaji hao kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fidia ili waweze kuondoka na kupisha mradi huo vinginevyo utasitishwa kuendelea na shughuli zake.

Dkt. Jafo ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kikazi kwa lengo kukagua na kujionea hali halisi, kujadili hatua stahiki zinazofaa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wanaozungukwa na mradi huo.

Sauti ya Dkt. Selemani Jafo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe amemshukuru Waziri Jafo kwa kufika katika eneo hilo kisha kusikiliza na kushughulikia changamoto hizo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe

Ameahidi kuyasimamia maelekezo yaliyotolewa na kuhakikisha wawekezaji hao wanatekeleza maelekezo hayo ndani ya siku 45 ambazo Waziri Jafo ametoa ili kuhakikisha madhara ya vumbi hayawafikii wananchi.