Dodoma FM

Tozo za mafuta na dizeli kujenga km 36 barabara wilayani Bahi

5 April 2023, 1:21 pm

kaimu Meneja wa TARURA wilayani Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Kukamilika kwa barabara hiyo ambayo inajengwa kwa kiwango cha changarawe kutachochea maendeleo ya wananchi wa maeneo hayo.

Na Benard Magawa

Zaidi ya shilingi Millioni 919 za Tozo ya mafuta ya dizeli na Petrol kutoka serikali kuu zinatarajia kukamilisha ujenzi wa barabara ya Mpunguzi mtitaa nkome yenye urefu wa kilomita 36 kwa pamoja na vivuko vyake ili kuondoa adha ya kujifunga kwa barabara hiyo pindi mvua zinaponyesha.

Hayo yamesemwa na kaima Meneja wa Tarura wilaya ya Bahi Mhandisi Malya ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo alipokuwa akizungumza na kituo hiki katika eneo la mradi na kueleze hali ya ujenzi wa barabara hiyo inayotarajiwa kukamilika mapema mwaka huu.

Amesema kukamilika kwa barabara hiyo ambayo inajengwa kwa kiwango cha changarawe kutachochea maendeleo ya wananchi wa maeneo hayo ambao wamekuwa wakipata adha kubwa ya barabara hususa ni wakati wa mvua ikiwemo kushindwa kusafirisha bidhaa mbalibali kupeleka mjini.

Sauti ya kaima Meneja wa Tarura wilaya ya Bahi .
kaimu Meneja wa TARURA wilayani Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Aidha ameeleza changamoto mbalimali katika kutekeleza mradi huo ikiwemo changamoto ya kukosekana kwa maji ya kutosha na kusema kuwa mkandarasi anaendelea kukabiliana nazo ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Sauti ya kaima Meneja wa Tarura wilaya ya Bahi