

4 April 2023, 6:18 pm
Hapa nchini pia hatua mbalimbali zimekua zikichukuliwa na serikali katika kuyahifadhi mazingira.
Na Fred Cheti.
Uhifadhi wa mazingira unatajwa kuwa ni moja ya hatua muhimu kutokana na kuwa rasilimali ardhi pamoja na kua nguzo kuu katika maendeleo ya nchi mbalimbali kote ulimwenguni.
Moja ya hatua zilizochokuliwa na serikali ikiwemo hapa jijini Dodoma ni udhibiti wa taka ngumu ambapo licha ya taka hizo kuonekana zikichafua mazingira pindi zinapotupwa hovyo lakini zimekua zitoa fursa kwa watu wengine wanaokota taka hizo na kuziuaza ili kujipatia kipato
Dodoma Tv imezungumza na Bwana Jabir Alhaji Mnunuzi wa taka ngumu ambapo hasa anaelezea jinsi ambavyo zitoa ajira kwa watu wengi na kusaidia katika utunzaji wa mazingira.
Nao miongoni mwa wananchi walioamua kutumia fursa hiyo ya kuokota taka ngumu wanaelezea jinsi ambavyo kazi hiyo ina manufaa kwao na kwa mazingira.