Dodoma FM

Bodi ya nafaka yaendelea kuimarisha soko la mazao Dodoma

4 April 2023, 5:35 pm

Upakuaji na upakiaji wa mazao ukiwa unafanyika . Picha na bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko.

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko imefanikiwa kununua  mazao ya wakulima yenye thamani ya Shilingi 9.6 Bilioni na kuzalisha Tani 480 zilizotolewa msaada Nchini Malawi.

Na Mindi Joseph.

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Mkoani Dodoma inaendelea kuimarisha Soko la wakulima  hususani katika zao la Mahindi, Mtama, Alizeti pamoja na Mafuta ghafi.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Meneja wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Lelansi Mwakibibi ambae amesema wanalenga kutengeneza soko la wakulima ili kuhakikisha hakuna urasimu wowote katika kununua mazao.

Sauti ya Meneja wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko
kiwanda cha kukamua mafuta. picha na Mindi Joseph.

Kwa upande wake, Afisa masoko Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tumpe manongi  amesema Bodi imekuwa  ikishirikiana na wakulima katika kuyaongezea thamani mazao.

Sauti ya Afisa masoko Mkuu