Dodoma FM

Wajasiriamali wanawake watakiwa kutengeneza bidhaa zenye ushindani wa soko

3 April 2023, 2:15 pm

Mafunzo ya utengenezaji wa sabuni bora za maji na vipande yaliyo tolewa kwa Wajasiriamali kutoka Taasisi ya wanawake na uchumi wa viwanda WAUVI. Picha na Alfred Bulahya.

Wajasiriamali hao wametakiwa kwenda kufanyia kazi mafunzo waliyo patiwa kwa kutengeneza bidhaa bora zenye kuleta ushindani katika soko.

Na Alfred Bulahya.

Wajasiriamali kutoka taasisi ya wanawake na uchumi wa viwanda WAUVI waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya utengenezaji sabuni za maji na vipande, wametakiwa kwenda kuzingatia mafunzo hayo kwa kutengeneza bidhaa bora na zenye ushindani sokoni.

Hayo yamesema na Mlezi  wa Tasisi hiyo Bi, Shufaa Mnyoty wakati akifunga mafunzo ya awali yaliyofanyika katika ukumbi wa sido kizota kwa muda wa siku tano.

Sauti ya Mlezi  wa Tasisi hiyo Bi, Shufaa Mnyoty
Wanawake hao wakiwa katika mafunzo ya ujasiriamali. Picha na Alfred Bulahya.

Aidha katika kuunga mkono juhudi za kukabiliana na changamoto zinazowakubwa wanachama hao akatoka kiasi cha shiling 50000 ili kuwasaidia kutimiza azma yao.

Mwenyekiti wa WAUVI mkoa wa Dodoma Rehema Nassoro akawa na haya ya kuzungumza

Sauti ya Mwenyekiti wa WAUVI mkoa wa Dodoma Rehema Nassoro

Mafunzo hayo yanayotolewa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo sido yamefanyika kwa muda wa siku tano na kwamba taasisi hiyo inatarajia kuanza kupatiwa mafunzo mengine ya utengenezaji wa Batiki na usindikaji wa Vyakula.